Leo ni Ijumaa Kuu, Polisi Wajipanga Kiulinzi

Leo ni Ijumaa Kuu, Polisi Wajipanga Kiulinzi

LEO ni Ijumaa Kuu siku ambayo wakristo duniani wanaungana pamoja kuadhimisha kifo cha Yesu Kristo, kabla ya maadhimisho ya siku Kuu ya Pasaka. Ibada ya kitaifa ya maadhimisho ya siku Kuu hiyo nchini Tanzania inatarajia kufanyika mkoani Dodoma katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Ijumaa Kuu ni siku ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za Mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa miaka 2000 iliyopita. Wakati huo huo Jeshi la Polisi nchini limewatoa hofu wananchi katika kusherehekea siku kuu hiyo, kwani limejipanga kuweka ulinzi mkali kuhakikisha usalama.

Kadiri ya Mtume Yohane kesho yake ilikuwa Sabato na pia Pasaka, jambo lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo wataalamu mbalimbali wanakadiria ilikuwa tarehe 7 Aprili 30. Ijumaa kuu pia ni sehemu ya Juma Kuu linaloanza kwa madhimisho ya Yesu kuingia mji huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (yaani Masiya au Kristo).

Ijumaa Kuu pia ni sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na kifo chake, kulala kaburini, na hatimaye kufufuka kwa utukufu. Mtandao wa dev.kisakuzi.com unawatakia Wakristo na Watanzania kwa ujumla maadhimisho mema ya siku hii ya Ijumaa Kuu.