Ligi kuu ya Uingereza imeendekea leo kwa michezo miwili ambapo Katika mchezo wa kwanza The Gunners wameambulia pointi moja baada ya kumaliza mchezo bila ya kufungana dhidi ya Sunderland
Katika mchezo mwingine Leicester City wameendeleza juhudi za kusaka taji la ligi hiyo baada ya kuilaza Swansea mabao 4-0. Mabao ya Leicester yamefungwa na Riyad Mahrez (10), Jose Leonardo Ulloa (30) na (60) huku la mwisho likifungwa na Marc Albrighton 85