Baadhi ya wananchi wakiwasaidia madereva wa pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda kunyanyua pikipiki zao baada ya kugongana wao kwenye makutano ya Mtaa wa Swahili na Barabara ya Pugu jana jijini Dar es Salaam.
Pichani madereva hao wakilaumiana wenyewe kwa wenyewe (aliyevaa kofia ngumu na flana nyeupe) kwamba kila mmoja akimuona mwenzake hakuwa makini. Baadaye walivutana pembeni na kuelewana nani amlipe nani kabla ya kuendelea na safari zao.