KVZ Yachapwa 2-0 na JKU Katika Ligi Kuu Ya Zanzibar

1
Wachezaji wa Timu ya JKU wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya KVZ kabla ya kuaza mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda 2–0.
Mchezo huo uliochezwa jana jioni huku mabao ya JKU yakifungwa katika kipindi cha kwanza na Mbarouk Chande pamoja na Nassor Mattar.
2
Beki wa timu ya KVZ Juma Abdalla, akijiandaa kumzuiya mshambuliaji wa Timu ya JKU mwenye mpira Nassorv Mattar, wakati wa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
3
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande, akimiliki mpira huku beki wa timu ya KVZ Emill William akijiandaa kumzuia.
4
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mohammed Abdalla akimpiga chenga golikipa wa timu ya KVZ Yakub Bakari. hatimai mpira huo na kutoka nje ya uwanja
5
Mshambuliaji wa Timu ya KVZ Masoud Abdalla mwenye jezi ya kijani akimpita mchezaji wa timu ya JKU Mbarouk Chande.