MSICHANA Kaden hakupenda yeye kuzaliwa jinsia hiyo. Hivyo baada ya kuanza kujitambua alianza mchakato wa kubadili jinsia yake. Taarifa za kisa hiki zilianza kusikika mwaka 2004, baada ya binti huyu akiwa na umri wa miaka 11 kukutana na kufanya mahojiano na muongozaji wa kipindi maarufu cha TV duniani ‘The Oprah Winfrey Show’, Bi. Oprah.
Alisema anahisi alizaliwa msichana kwa makosa hivyo anafikiria kufanya mabadiliko ya kubadili jinsia yake na kuwa mvulana. Alisema ataanza kufanya mabadiliko hayo atakapotimiza miaka 18 wakati yu umri wa mtu mzima.
“…Vitu vizuri vilijitokeza na mara nyingine vibaya vilijitokeza katika hatua mbalimbali za mimi kubadili jinsi yangu…kulikuwa kuna vitisho na shinikizo la vikwazo lakini nilifanikiwa, sasa ninafuraha kuwa hivi nilivyo (mvulana),” anasema Kaden akihojiwa na Oprah.
Anasema akiwa na umri wa miaka 14, alianza kutumia dawa zinazoamsha homoni za kiume kama ‘testosterone gel’ na baadaye aliendelea na matumizi ya kemikali hizo hadi alipotimiza miaka 16. “…Kimsingi nilianza kuona mabadiliko hasa kwenye mishipa yangu, pia ngozi yangu ilianza kuota nywele nyingi na sauti ilibadilika kama mwanaume,” alisema Kaden.
Baada ya hapo nikiwa na umri wa miaka 16 nilikwenda kufanyiwa upasuaji wa kifua na kuondolewa matiti ya kike, na kutengenezwa kuwa mwanaume. “Nakumbuka nilijihisi nipo fiti wakati huo, kutokana na mabadiliko kuanzia ngozi na hata kiakili…ule uigizaji wa jinsia ulianza kupotea na kuwa halisia,” anasema Kaden.
But deciding whether to have genital reconstruction surgery is another story. Though Kaden Hata hivyo kufanyiwa upasuaji mkubwa kwa ajili ya kubadili viungo vyake kuwa kama anavyojisikia ni kitu kingine. Anasema hilo limemkatisha tamaa baada ya kufanya mazungumzo na daktari. Anasema kinachomuumiza zaidi ni baada ya madaktari kumjuza kuwa licha ya kuwekewa viungo anavyovitaka havitafanya kazi kama ilivyo kwa wengine.
“…Sikuwa na furaha kabisa baada ya kuambiwa viungo vyangu hivyo endapo nikibadili havita fanyakazi, vitakuwa hivyo kwa mtazamo tu lakini sitaweza kuwashughulikia wasichana kama wezangu,” anasema kwa hudhuni Kaden.
Sijui kama nitakuwa na moyo wa kuendelea na fikra zangu, kama nitabadili lakini kushindwa kuvitumia viungo hivyo kama ninavyotaka vitakuwa na umuhimu gani? Anasema katika mchakato wake wa kubadili jinsia aliwahi kuwa na mahusiano na mwanamke mmoja yeye akiwa kama mwanaume alifanya hivyo na pia kuweka wazi kwa rafiki yake huyo mpenzi, aliridhia na kumkubali.
Wataka kujua binti huyu anayetaka kuwa mwanaume ameishia wapo fuatana nasi wiki ijayo kumalizia stori yake hapa hapa www.thehabari.com…