Kush Lodhia Aibuka Kidedea ‘Rhino Automobile Services golf’

Thehabari.com
Bertha Ismail, Arusha

MPIGA gofu Kush Lodhia ‘week end’ hii ameibuka kidedea katika michuano ya “Rhino Automobile Services golf” baada ya kujipatia alama 38 katika miduara 18 ya mchezo wa gofu yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkana jijini Arusha.

Michuano hayo yaliyoshirikisha wachezaji 50 wa gofu kutoa Arusha kati yao watoto wanne walishiriki na wasichana watatu, ambapo mbali na ushindi wa jumla wa Lodhia pia aliongoza kundi la daraja la kwanza akifuatiwa na Izack Wanyeche alishika nafasi ya pili kwa alama 38 na kuzidiwa penalt.

Daraja la pili Hussein Kermali alishika nafasi ya kwanza kwa alama 39 baada ya kumpiku Monu Sigh kwa penalt ambae nae ana point 39 na daraja la tatu Jamali Mukarram aliongoza kundi na kufuatiwa na Harbajan Chadha aliyejikusanyia alama 38.

Mpiga gofu wa kimataifa Madina Iddi alifanikiwa kuwapiku wanawake wenzie na kuibuka mshindi kwa alaman 32 huku kwa wazee Peka Niskala akiongoza kwa alama 35 na kwa watoto Aliraza Kermalli aliibuka kidedea.

Akizungumza baada ya michuano hiyo, Mdhamini wa michuano hayo Arif Bhimani ambae ni mkurugenzi wa kampuni ya Rhino Automobile Services Ltd inayojishughulisha na uchunguzi, utengenezaji na uwekaji wa kiyoyozi kwenye magari ya aina zote (Body work, diagnostic for high and Vihicles, A/C servicing, penal beating and Spray painting n.k) alisema amevutiwa na mashindano hayo na kuahidi kuendelea kuyadhamini ili kuwapa wachezaji motisha ya kucheza gofu zaidi.

“Michuano haya ya mara kwa mara ni mazuri kwani mbali na kukuza mchezo wa gofu lakini pia inazidi kuwanoa wachezaji hawa ambao si wataalam wa mchezo huu kuzidi kuwa na makali hasa katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye michuano ya kimataifa,”