Kura rasmi za urais DRC kucheleweshwa


TUME ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema itachelewa kutangaza matokeo rasmi ya kura za urais kutokana na matatizo ya usafirishwaji wa nakala za kujumlishwa kwa kura.

Taarifa zinasema matokeo ya awali yanaonesha rais wa sasa, Joseph Kabila (pichani juu) anaongoza akiwa mbele ya wapinzani wake ambao tayari umesema hautamtambua kiongozi huyo kama rais baada rais wa Congo.

Tume ya uchaguzi iliomba msaada wa helikopta za Umoja wa Mataifa kusafirisha karatasi za kujumlisha kura huku makarani wa kujumlisha kura za taifa mjini Kinshasa wakiwa mbioni kumaliza hesabu yote kabla ya Jummanne. Hata hivyo masanduku ya kura ambazo hazikujumlishwa yalikuwa bado kufunguliwa hapo jana.

Ofisa mmoja wa kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi amesema upande wake hautamtambua rais Kabila baada ya kipindi chake kumalizika chini ya katiba ya taifa.Wakati huo huo polisi wa kuzima ghasia wamekabiliana na wafuasi wa bwana Tshisekedi mjini Kinshasa. Shughuli za kawaida zimekwamishwa na taharuki zilizoko katika maeneo mengi nchini humo.
-BBC