LEO Watanzania wanaadhimisha miaka 12 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyefariki tarehe kama ya leo mwaka 1999. Nyerere ambaye alikuwa muhimili wa Taifa la Tanzania alifariki Oktoba 14, 1999 katika hospitali ya St. Thomas ya London, Uingereza.
Kiongozi huyu atakumbukwa milele kutokana na uadilifu, msimamo kimaamuzi, ujasiri na uwezo mkubwa wa uongozi aliokuwa nao wakati wa uhai wake. Nyerere aliendelea kuwa muhimili hata alipostaafu masuala ya siasa, kwani ushauri wake ulionekana kuhitajika kiasi kikubwa. Uongozi na timu nzima ya dev.kisakuzi.com inaungana na Watanzania wote kumkumbuka Baba wa Taifa leo na siku zote. Amin.