Kumbe tuna International Schools za kata Tanzania!

Jengo la utawala na ilipo maktaba ya shule ya kata ya Kaloleni lilojengwa kwa ufadhili wa JICA


Sayansi bila vitendo haiwezekani, shule hii ina maabara za masomo yote matatu ya baiolojia, fizikia na kemia.


Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Mrs Machange M. J akifanya mahojiano na mwandishi


Maelezo ya sehemu mbalimbali zinazopatikana katika shule hii


DHANA ya kwamba shule zote za kata ziko katika mazingira magumu na hazifanyi vema katika maendeleo ya elimu si sahihi kwani kuna baadhi ya Shule za Sekondari za Kata ambazo zina maendeleo mazuri sana kitaaluma kushinda hata zile shule Kongwe za Serikali na Shule nyingi za binafsi. Fuatana na mwandishi wetu Abraham Lazaro wa Shirika la HakiElimu aliyefanya ziara hivi karibuni katika Wilaya ya Arusha na kuitembelea Shule ya Kata ya Kaloleni.