MKUU wa Kampuni Maarufu Duniani na Tajiri ya Apple, Tim Cook ametangaza kuwa yeye ni shoga. Bilionea huyo Cook alisema anajivunia kuwa shoga. Cook alitoa tamko hilo kujaribu kuwasaidia watu wanaong’ang’ana kutangaza jinsia zao katika ripoti iliochapishwa na gazeti la biashara la kila wiki la Bloomberg.
Alisema mbali na kuweka wazi hivyo, lakini pia amejaribu kuweka maisha yake katika faragha kwa muda hadi sasa alipoweka wazi. Wiki hii Cook alitoa changamoto kwa Jimbo lake la Alabama kuhakikisha kuwa haki za mashoga na wale wanaobadili jinsia zinaheshimiwa.
“Mimi sijitambui kama mwanaharakati, lakini nimegundua nilivyofaidika na mikakati iliowekwa na wengine,” alisema Cook. “Kwa hivyo iwapo watu wakisikia kwamba mimi ni shoga kutawasaidia baadhi yao, ama kumpa faraja yule anayejisikia mpweke ama kuwashinikiza wengine kupigania haki zao, basi afadhali kutangaza maisha yangu ya faragha,” aliongezea.
Bilionea Cook alisema amekuwa wazi kuhusu jinsia yake na watu wengi wakiwemo wafanyikazi wenzake katika kampuni ya Apple, lakini hilo halikuwa chaguo rahisi kutangaza hadharani kuhusu jinsia yake.
-BBC