ZAKARIA Antony Mwiru ni kijana aliyekuwa m-bwia unga awali na anafafanua zaidi katika mahojiano.
MO BLOG: Tupe histioria fupi ya maisha yako..!
MWIRU: Naitwa Zakaria Antony Mwiru nikiwa mzaliwa wa Kusini mwa Tanzania lakini wazazi wangu walihamia Dar es Salaam nikiwa na umri wa miaka 2, hivyo nimekulia Dar es Salaam na kusoma Shule ya Msingi Kinondoni A na Nikasoma Shule ya Sekondari Kinondoni Muslim mpaka Kidato cha 4 bahati mbaya nilifeli hivyo nikajiunga na Chuo cha Sanaa Bagamoyo kwa muda wa miaka 3 nikasoma sanaa za ‘Wood Carvings’, ‘Sculpture’, ‘Painting’ na ‘Ngoma za Utamaduni’.
Baada ya kuhitimu kwa miaka mitatu nilifanya shughuli zangu za sanaa kwa muda wa kama miaka mitano hivi, na baadae nikajikuta nimeingia katika sakata la dawa za kulevya.
MO BLOG: Badala ya kuendelea na sanaa uliyojifunza Bagamoyo ilikuaje ukaingia katika mkumbo wa matumizi ya dawa za kulevya.
MWIRU: Nahisi sababu iliyonivutia kuingia kwenye mkumbo wa dawa za kulevya ni kutohisi kuwa na furaha kwa maisha ninayoishi na nikategemea kwamba nitapata furaha zaidi kama nitatumia ulevi, kwa hiyo nikaanza na bangi kisha pombe na baadae nikaingia katika matumizi ya Heroin. Lakini vile vile sikupata ile furaha niliyokuwa naitegemea na matokeo yakawa mabaya zaidi na baada ya muda mrefu nilichoshwa na ile hali iliyojaa mateso ndani yake. Kusoma Mahojiano yote Bofya hapa.
Kusoma zaidi tembelea; www.mohammeddewji.com/blog