Kongamano la Jumuia ya Wafanyabiashara Wanawake Lafanyika Dar

Mmoja wa majaji akiangalia bidhaa mbalimbali zilizopangwa kwenye meza zilizotokana na ubunifu wa wanawake waliohudhuria kongamano hilo.

Mmoja wa majaji akiangalia bidhaa mbalimbali zilizopangwa kwenye meza zilizotokana na ubunifu wa wanawake waliohudhuria kongamano hilo.

 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women,  Haika Lawere akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Guarden Dar es Salaam.
 
 Mwezeshaji wa Kongamano hilo, James Mwang’amba 
akitoa mada.
 Muwezeshaji wa kongamano hilo, Chriss Rupia (kulia), akitoa maelezo juu ya namna ya kuanzisha Kampuni na hatua mbalimbali ambazo mtu anatakiwa azifuata wakati wa kufungua kampuni hasa binafsi.
 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women Haika Lawere (wa kwanza kulia) pamoja na wadau wengine wakiangalia bidhaa mbalimbali wakati wa kongamano hilo. 
Baadhi ya wajasiriamali na wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano hilo.
Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo Getrude Kilyabusebu (Kulia) akiweka sawa  kumbukumbu ya wadau waliofika katika kongamano hilo.
Bidhaa mbalimbali zikioneshwa.
Maonyesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea.

 

Baadhi ya wajasiriamali wakionesha kazi zao.
  Wadau mbalimbali wakitizama bidhaa mbalimbali katika Kongamano hilo.



Na Dotto Mwaibale



WAJASIRIAMALI wanawake nchini wametakiwa kuwa na moyo wa uthubutu ili kupiga hatua ya maisha na kiuchumi badala ya kuwa waoga.



Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Kongamano la Jumuia ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, Julieti Mjale wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam jana.



“Uthubutu katika jambo lolote ni muhimu kwani unamfanya muhusika kupiga hatua ya maendeleo” alisema Mjale



Alisema wajasiriamali waliowengi wamekuwa na mipango mizuri ya kubuni biashara fulani lakini wanakuwa na hofu ya kupoteza fedha zao na hiyo inatokana na kushindwa kuthubutu au kuchukua maamuzi magumu ya kuanza kufanya biashara waliyoikusudia.



Akijitolea mfano yeye alisema alithubutu kwa kuanza kufanya biashara za chini lakini leo hii ana nyumba za kupangisha na kufikia hatua ya kufanya biashara za kwenda nje ya nchi na kuandaa makongamana ya namna hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara.



Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Haika Lawere alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wajasiriamali wanawake ili kupeana uzoefu wa biashara na kujua changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.



Katibu wa Jumuia hiyo, Hilda Ngaja, alisema changamoto kubwa waliyonayo wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na uelewa mkubwa wa kufanyabiashara zao na kujikuta wakirudi nyuma kimaendeleo na ndio maana wamekuwa wakitumia fursa za semina na makongamano kwa ajili ya kuelimishana.

(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)