Komando Kalala Afanya Mazungumzo na Ras Makunja

Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa Band na Komando hamza Kalala ndani Sibuka FM jijini Dar es Salaam.

Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa Band na Komando hamza Kalala ndani Sibuka FM jijini Dar es Salaam.


HIVI karibuni ndani ya studio za Sibuka FM, kwenye kipindi cha Pepeta Afrika, mgeni na nyota wa wiki alikuwa ‘Kamanda’ Ras Makunja kiongozi wa bendi maarufu barani Ulaya Ngoma Africa a.k.a FFU Ughaibuni au Anunnaki Alien pia waweza kuwaita ‘Watoto wa Mbwa’. Ras Makunja katika mahojiano hayo aliambatana na mkongwe wa muziki nchini Komandoo Hamza Kalala.

Kamanda Ras Makunja katika mahojiano yake na TV na Redio Sibuka, na alizungumuzia zaidi nafasi ya
muziki wa dansi wa Tanzania katika masoko ya kimataifa. Mwanamuziki huyo wa Tanzania mwenye makao yake nchini Ujerumani alitoa wito kwa Watanzania waishio ndani na nje ya nchi kuzipa nafasi bendi za muziki za Tanzania ili ziweze kuvusha muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na kufanya ziara za kimataifa.

Ras Makunja aliutaja muziki wa dansi wa Tanzania “Bongo Dansi” kuwa una nafasi kubwa katika soko la kimataifa hiwapo Watanzania wenyewe watakuwa mstari wa mbele katika kuutanga na kuzipendekeza bendi za Tanzania kwa maporomota na waandaaji wa maonyesho ya kimataifa.

Ras Makunja aliongozwa na mwanamuziki mkongwe nchini Komandoo Kalala ambaye aliutaja muziki wa Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni kuwa ni muziki ulipangiliwa kwa mtindo wa kushambulia na kuteka washabiki katika masoko. Komando Hamza Kalala alimtaja Kamanda Ras Makunja kuwa ni mojawapo wa wanamuziki wachache wa kitanzania wanao ipeperusha bendera ya Bongo kimataifa bila ya uwoga.
Usikose kuwasikiliza FFU wa Ngoma Africa band at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com