Mwanamuziki nguli Barani Afrika kutoka nchini Congo Charles Koffi Olomide ameipongeza kampuni ya bia SBL kupitia kinywaji chake cha Tusker kwa kuonyesha kuwajali na kuwathamini wateja wake.
Olomide amesema ujumbe unaotolewa na kampuni hiyo”kunywa kwa uangalifu na usiendeshe gari ukiwa umelewa” ni ujumbe ambao unaonyesha SBL mbali na kuangalia maslahi unamjali mteja.
Koffi ametoa kauli hiyo leo mchana jijini Dar alipokuwa na mkutano na wanahabari amesema ” Nimependa ujumbe unaotolewa na Tusker kwa wateja unaonesha kampuni hii inavyo wajali na kuwathamini wateja wake si biashara tu” alisema Koffi.
Awali mkurugenzi wa masoko wa SBL Efraim Mafuru alisema Tusker imemleta gwiji wa muziki wa dansi Afrika hili kutii kiu ya wapenzi wa bia hiyo nchini.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na viongozi wajuu SBL,Clous Fm na Maofisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani.