
Kocha wa mchezo wa ngumi, Rajabu Mhamila ‘Super D’ kushoto akimkabidhi zawadi ya clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K’O raundi ya pili, bondia huyo ndiye bingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam na anajiandaa na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu.

Kocha Mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwinua mkono juu bondia Mussa Mchopanga baada ya kumvalisha medali ya Dhaabu baada ya kuibuka mshindi wa Mkoa wa Dar es Salaam.