Kocha wa Leicester City Atoa Machozi Uwanjani

download

Meneja wa timu ya Leicester City Claudio Ranieri alibubujikwa na machozi baada ya kufurahishwa na vijana wake walipoitandika Sunderland kwa mabao 2-0

Ushindi huo uliongeza uwezekano wa timu hiyo kutawazwa mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo, baada ya kufungua mwanya wa pointi 7.

Alikuwa Jamie Vardy aliyeipa ushindi Leicester kwa kupachika mabao mawili muhimu jana Jumapili.