Kocha Mkwasa Awashukuru Watanzania, Kozi ya Makocha Julai 13

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa akizungumza na waandishi  wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.


KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa amewashukuru watanzania wote waliowapa sapoti katika mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda uliochezwa mwishoni mwa wiki jijini Kampala.

Mkwasa amesema kujitolea kwa wachezaji wa Taifa Stars (uzalendo) katika mchezo huo kulipelekea kuwapa wakati mgumu wenyeji, huku watanzania waliojitokeza kuja kushuhudia mchezo huo wakiwashangilia muda wote wa mchezo.

“Kiukweli japo timu haikuweza kupata matokezo mazuri sana, lakini tunamshukuru mungu ndani ya wiki moja ya maandalizi, tumeweza kuwapa maelekezo vijana na kuyafanyia kazi, japo wengine walikua wakicheza kwa mara ya kwanza timu ya Taifa walicheza vizuri, kijumla wote kwa pamoja walifanya vizuri sana katika mchezo dhidi ya Uganda” alisema Mkwasa.

Aidha Mkwasa amesema kwa sasa wataomba kupata nafasi ya japo siku 10 kufanya mazoezi kwa pamoja kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Nigeria Septemba 5 mwaka huu, na kuwaomba watanzania wote kuwaunga mkono katika maandilizi hayo.

CECEFA KAGAME CUP MEDIA ACCREDITATION
Maombi ya vitambulisho vya waandishi wa habari kwa ajili ya michuano ya CECAFA Kagame Cup 2015 yamefunguliwa rasmi kuanzia leo tarehe 7 Julai, 2015 katika tovuti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF.

Kila Kampuni ya Habari (Media House) inaombwa kuomba vitambulisho vitano (5) vya waandishi wa habari watakaofanya kazi wakati wa michuano ya kombe la Kagame Cup kwenye tovuti ya TFF (tff.or.tz) kisha kuchagua KAGAME CUP, ACCREDITATION na kujaza fomu ya maombi ya kitambulisho na kuambatanisha na picha ya muombaji.

Mwisho wa kuomba kitambulisho kwa waandishi wa habari ni jumatano tarehe 15 Julai, 2015 saa 6 kamili usiku. Waombaji wa vitambulisho hivyo wote wanaombwa kufanya maombi hayo mapema ili kuondokana na usumbufu wakati michuano ya Kagame itakapokua imeanza. Fuata link hii kujaza maombi ya kitambulisho

http://tff.or.tz/kagame-cup-2015/accreditation

Katibu wa Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine akiwa na makatibu wa vyama vya soka nchini.

Katibu wa Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine akiwa na makatibu wa vyama vya soka nchini.


KOZI YA MAKOCHA WA MAGOLIKIPA JULAI 13
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF litaendesha kozi ya makocha wa magolikipa nchini itakayofanyika Julai 13 – 17, 2015 jijini Dar es salaam

Jumla ya makocha wa magolikipa 29 wanatarajiwa kuhudhuria kozi hiyo itakayofanyika katika ofisi za TFF zilizopo Karume. Orodha ya Makocha watakaohudhuria kozi hiyo na timu wanazotokea kwenye mabano ni Rafael Mpangala (Mgambo JKT), Adam Abdallah Moshi (Simba SC ), Khalid Adam Munnisson (Mwadui FC), Choke Abeid (Toto African), Mussa Mbaya (Ndanda FC), Idd Abubakar Mwinchumu (Azam FC), Herry Boimanda Mensady (Tanzania Prisons), Kalama Ben Lwanga (Stand United), Patrick Mwangata (Mtibwa Sugar), Juma Pondamali (Young Africans).

Wengine ni Abdi Said Mgude (Coastal Union), Razack Siwwa (African Sports Tanga), Josia Steven Kasasi (Mbeya City), Ramadhani Juma (Kagera Sugar Kagera),Abdallah Said Ngachimwa (JKT Ruvu), John Bosco (Majimaji FC Ruvuma), Fatuma Omary (Twiga Stars), Juma Kaseja Juma (Premier League), Athuman Mfaume Samata (Ilala), Peter Manyika John (Taifa Stars).

Hussein Tade Katadula (African Lyon), Juma Mohamed Bomba (Kinondoni), Mwameja Mohamed Mwameja (Ilala), Agustino Malindi Mwanga (Kigoma), Mohamed Abbas Silima (Police SC. Zanzibar), Bakari Ali Kilambo (Kizimbani SC Zanzibar), Hafidh Muhidin Mcha (Zanzibar Heroes), Elyutery Deodatusy Mholery (Kinondoni), Salim Waziri (Tanga)
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)