Klopp amwonya Guardiola kuhusu Ligi ya Uingereza

kloop

Kocha wa Liverpool Jürgen Klopp amemwonya Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu msongamano wa orodha ya michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza

Guardiola ambaye tayari kajiunda na Manchester City na tangu kocha huyo wa zamani wa Barcelona alipothibitisha kuwa anaondoka Bayern mwishoni mwa msimu huu na anaelekea England.

Klopp alisema kila kitu England, ni kandanda, kandanda, kandanda. Ukiwa na maandalizi mazuri ya kabla ya kuanza msimu, unakuwa na safari ndefu ndefu sana. Nnachoweza kusema kuhusu Uingerea ni uwe na matumaini, ni nchi nzuri, watu wazuri, chakula ni kizuri sana kuliko ilivyosemwa na kila mtu.