HOSPITALI maarufu za kimataifa za Apollo ambazo zimeazimia kufungua hospitali na kliniki mbali mbali nchini, hivi karibuni zimetangaza uamuazi wake wa kushirikiana na Sanofi katika upanuzi wa Kliniki za Kisukari za Apollo ambazo zinatatoa huduma jumuishi kwa wagonjwa wa kisukari nchini India. Watanzania wanatazamia kufaidika kutokana na uhusiano uliopo kati ya nchi ya Tanzania na hospitali za Apollo kwahuduma zinazotolewa kwa wagonjwa wanaoenda kupata matibabu nchini India.
Kupitia uhusianoi huo, Apollo na Sanofi wameratibu kutumia ujuzi walionao kwenye masuala ya ugonjwa wa kisukari kutoa huduma bora kupitia elimu, matibabu na mipango itakayosaidia wagonjwa wa kisukari kupata ahueni. Hatua ya kwanza ya uhusiano imelenga kuanzisha kliniki za kisukari hamsini (50) kote nchini India.
Magonjwa yasiyoambukizwa hupelekea vifo vya watu milioni 36 kila mwaka ambvyo ni sawa asilimia 80% vingi vikirekodiwa katika nchi zenye vipato vya chini na kati. Zaidi ya hayo, mzigo wa kiuchumi nchini Tanzania unaosababishwa na hasara itokanayo na magonjwa ya kisukari na moyo inafikiriwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa zaidi ya bilioni 2.5 za dola za Kimarekani kati ya 2005 na 2015. Nchini Tanzania, magonjwa yasiyoambukizwa hupelekea asilimia 31% ya vifo vya watu kulingana na takwimu zilizotelewa na shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye takwimu za nchi mbali mbali duniani.
Shirikisho la Kimataifa la Kisukari (IDF) linakadiria watu milioni 382 duniani walio na ugonjwa wa kisukari ikiwa zaidi ya watu milioni 19 kutoka bara la Afrika wakati kesi za takriban watu 1,706,930 wenye kisukari zimeripotiwa mwaka 2013.
Katika jitihada za kudhibiti ushamiri wa janga la kisukari duniani, Kliniki za Kisukari za Apollozimelenga kuondoa maradhi yatokanayo na ugonjwa wa kisukari kwa kutoa huduma rahisi na bora ndani ya kliniki itakayopelekea ugunduzi wa mapema na tiba mbadala kwa wagonjwa wa kisukari na matatizo yatokanayo na ugonjwa huo, na mfumo bora wa maisha na mabadiliko ya tabia.
Akizungumzia uhusiano huo, Dkt. Dr. Prathap Reddy, Mwenyekiti – Apollo Hospitals Group shared, “Kwa muda mrefu, Hospitali za Apollo zimeongoza duniani katika kutoa huduma bora za afya kulingana na viwango na taratibu za huduma za afya. Na ongezeko la ugonjwa wa kisukari, jamii inabidi kufanya maamuzi haraka yenye nia kutokomeza ugonjwa huu unaosababisha vifo vya watu wengi. Ni Imani kwamba kupitia Kliniki za Apollo tutafanikiwaw to kuwapa wagonjwa wa kisukari huduma za kisasa na ushauri ambao utawasaidia kuangalia afya zao. Huu ni mwanzo mzuri katika kuboresha miundo mbinu ya kutibu kisukari. Ndoto yetu ya pamoja itasaidia kufanya njia mpya za kuhudumi wagonjwa wa kisukari ambayo inatafaidisha wagonjwa hao.”
“Sanofi ina takriban miaka 100 ya urithi katika masuala ya kuendeleza matibabu ya kisukari na inafahamu shinikizo walilonao wataalamu kwa wagonjwa wanaoangalia afya zao za kisukari alisema Christopher A. Viehbacher, Afisa Mkuu Mtendaji, Sanofi.” Kwa kuungana pamoja na kuanzisha Kliniki za Kisukari, Sanofi na Apollo wanaonyesha jitihada zake kwa wagonjwa wa kisukari zinazotoa mchango kwa kila hatua ya ugonjwa wa kisukari ili kupunguza mzigo.
Huku kukiwa na ongezeko la watu wanaougua kisukari duniani, wagonjwa wengi bado hawatambui hali zao za kiafya ama kutoangalia hali zao vizuri. Wagonjwa hawa wanahitaji uelewa kuhusu ugonjwa huu na kupata huduma za kisasa. Katika mawazo haya,Sangita Reddy, Mwenyekiti, Apollo Sugar na Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali za Apollo, alisema “Apollo imetambuliwa na American Diabetes Association kwa utoaji wa huduma wenye mafanikio kwa wagonjwa wa kisukari kwa mara ya kwanza nchini India. Lakini, kama taifa bado tunapambana kutambuliwa kama senta ya kisukari duniani. Tunatambua kuwa kugundulika na ungonjwa wa kisukari na kulazimika kubadili mwenendo wa maisha huogopesha wagonjwa, hivyo, tumedhamiria kuwasaidia wangonjwa kupata ushauri na matibabu sahihi. Katika kliniki hizi wagonjwa wa kisukari wataweza kujipatia habari, ushauri na matibabu na uangalizi. Tumedhiria kupeleka huduma sehemu nyingi.”
Kliniki ya Sukari ya Apollo ni sehemu ya tawi la Apollo Health & Lifestyle ambalo linachangia kwa kasi katika ukuaji wa afya. Kama ilivyo kwa wagonjwa wa kusikuri nchini India, hali kadhalika kwa wangonjwa wa kisukari nchini Tanzania hutumia pesa nyingi kwa mwaka kupata matibabu ikiwa ni kiasi cha dola za kimarekani $31 wakati hatua za mwisho za ugonjwa hugharimu mara 10 hadi 18 zaidi. Gagan Bhalla, Afisa Mkuu Mtendaji, Apollo Sugar alimalizia kwa kusema, “Aina hii ya gharama inaweza kusababisha athari kubwa za kiuchumi kwa familia na hata kupelekea madeni. Katika kliniki yetu tunaamini kuwa kwa huduma bora na kisasa, na uangalizi wa karibu wa mienendo kwa wa wagonjwa wa kisukari italeta matokeo mazuri katika.”
Kuhusu Apollo
Mnamo mwaka 1983, Dk. Prathap C Reddy, mtaaalamu wa afya nchini India, alianzisha mlolongo wa Hospitali za Apollo Chennai. Hospitali za Apollo zimekua miongoni mwa hospitali kubwa katika bara la Asia likiwa na vitanda 8,500 vya wa wagonjwa katika hospitali zake 50, na zaidi ya maduka ya madawa 1,350 na zaidi ya kliniki za uchunguzi 100.
Mkusanyiko wa hospitali hizo pia unatoa huduma za medical business process outsourcing services, bima za afya na kliniki za research katika masuala ya epidemiological, stem cell research na genetic research. Ili kuendeleza utoaji wa huduma za afya, Hospitali za Apollo zina vyuo 11 vya mafunzo ya unesi na menejimenti za hospitali. Mafanikio haya yamepelekea tuzo mbali mbali kama Centre of Excellence from the Government of India and recognition from the Joint Commission International kwa hospitali saba za Apollo.
Pia serikali ya India ilitoa tuzo ya commemorative stamp kwa kutambua mchango wa Hospitali za Apollo katika kutoa huduma za afya. Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo alipewa tuzo Mashuhuri ya prestigious Padma Vibhushan, mwaka 2010. Kwa miaka 30 Hospitali za Apollo imefanikiwa kudumisha na huduma ya afya na madawa, kliniki za kisasa na teknolojia ya hali juu. Hospitali zetu ni miongoni mwa hospitali bora duniani kwa huduma za afya za kisasa na utafiti.