Na Mwandishi Wetu
WANAHBARI maalumu watakao ripoti Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji wameanza kunolewa leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
Akizungumza leo wakati akifungua Kliniki hiyo Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye alisema vyombo vya habari ni nyenzo muhimu katika utoaji wa taarifa yoyote.
Alisema CECAFA kwa kutambua umuhimu huo imeamua kuwakutanisha wanahabari na kujaribu kukumbushana masuala muhimu kwa maslahi ya wadau wote wa soka wanaojumuika kufanikisha mashindano.
“Bila vyombo vya abari hatuwezi kufanikiwa katika soka, nyinyi ndio kila kitu. Mnapokea taarifa na kuwajuza wananchi nini kinaendelea kwenye mashindano na masuala mengine, kwa hiyo tunawategemea na mnapaswa kutambua kuwa mnaumuhimu mkubwa,” alisema.
Naye Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Saadi Kawemba alisema wanatambua umuhimu wa wadhamini wote wanaojitolea kufanikisha mashindano hayo (Serengeti Breweries-SBL mdhamini Mkuu na Mradi wa Kupambana na Malaria nchini) na kuomba waungwe mkono kimafanikio zaidi.
Akizungumzia mgonjwa wa maleria Kawemba alisema kuna kila haja ya kima mmoja kushiriki kikamilifu katika kupambana na ugonjwa huo kutokana na madhara makubwa yaliopo.
Alisema kila familia inaathirika na ugonjwa huo na kila familia ndani kuna mchezaji mmoja ama mtarajiwa au anaecheza kwa sasa, haina budi kila familia kushiriki katika mapambano hayo.