
Mmoja wa wachezaji nyota wa mpira huo kutoka ligi ya Marekani (mbele kushoto) akitoa maelekezo kwa vijana wanaohudhuria mafunzo hayo.
KLINIKI ya mafunzo ya mpira wa kikapu nchini kwa vijana kutoka mikoa 16 ya Tanzania imeanza leo ndani ya viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanatolewa na nyota watatu wa mpira wa kikapu kutoka ligi ya nchini Marekani.
Wachezaji ambao wanaendesha Kliniki hiyo ni Tamika Raymond (WNBA), Becky Bonner (WNBA) na Dee Brown (NBA) aliyechezea , Dallas Mavericks ambao kwa pamoja ni wachezaji nyota mchezo huo katika ligi za Marekani. Zifuatazo ni picha mbalimbali za Klinik hiyo:-