Balozi wa Marekani nchini Tanzania kuifungua
Na Moshi Stewart, MAELEZO-Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini na wadau wengine kama Coca-Cola kupitia kinywaji cha Sprite na Family Healthy International (FHI), wameandaa ziara ya kimichezo ya mafunzo ya ‘Basketball’ yatakayotolewa na wachezaji wa zamani wa ligi kubwa ya mpira wa kikapu duniani ya NBA na WNBA
Taarifa hiyo imetolewa leo na Makamu Rais wa TBF, Phares Magesa ambapo amewataja wachezaji watakaokuja kuwani ni Tamika Raymond (WNBA), Becky Bonner (WNBA) na Dee Brown (NBA) aliyechezea , Dallas Mavericks na wachezaji nyota mchezo huo ligi za Marekani
Akifafanua, Phares amesema msafara huo wa wachezaji ndio watakaotoa mafunzo katika kliniki iliyoandaliwa nchini na wanawasili leo Septemba 5, 2011 saa 12:50 jioni na kuanza kutoa mafunzo Septemba 6, 2011 hadi 8, 2011.
Aidha alisema mafunzo hayo yatafunguliwa na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt saa 2:30 asubuhi, katika viwanja vya Don Bosco, Upanga. Aliongeza kuwa kliniki ya mwaka huu ni ya tofauti kidogo na zilizofanyika miaka ya nyuma kwani itawakutanisha vijana zaidi ya100 walio na umri chini ya miaka16 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Akiitaja mikoa hiyo ni Dar-es-Saalam, Kagera, Mara, Tabora, Mtwara, Ruvuma, Singida, Visiwa vya Zanzibar, Shinyanga, Kigoma, Iringa, Rukwa, Lindi na Kilimanjaro ambapo kila mkoa utawakilishwa na vijana 3 waliochini ya umri wa miaka 16 wa kike na kiume na Mwalimu 1 wa kikapu.