Kiwanda cha Konyagi Chalalamika Kuchafuliwa na Magazeti

MKURUGENZI Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, ambapo alilalamikia kitendo cha baadhi ya magazeti yenye uhusiano wa nchi jirani, yanayotumika kuchafua bidhaa za TDL.

MKURUGENZI Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa jana jijini Dar es Salaam amelalamikia kitendo cha baadhi ya magazeti nchini ambayo amedai yana uhusiano wa nchi jirani yameyokuwa yakitumika kuchafua bidhaa za kampuni yao (TDL). Kiongozi huyo ametoa tamko hilo alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

“Tumeanza kuona magazeti yenye affiliation na nchi za jirani yakitumika ku misrepresent products za TDL.
Articles ninazozungumzia zilichapishwa tarehe 2 may 2013 na tarehe 6 may 2013, kupotosha umma, na kupindisha ukweli. kwa sababu mawasiliano ya kisheria yanafanyika sitataja ni magazeti gani yanahusika, lakini nina uhakika yana uhusiano mkubwa wa kibiashara na nchi jirani.”

Ushauri wangu ni kuwa magazeti ya Tanzania, yaepukane sana na vitu vinavyoonyesha kuwa kuna muelekeo wa kurepresent matakwa ya nchi tofauti na kupuuza matakwa ya kitanzania Kitendo cha kujaribu kuoanisha brand ya Konyagi na accidents za magari au piki piki, ni ya upotoshaji mkubwa wa jamii ya kitanzania, kwani hakuna bia, hakuna pombe za kienyeji au pombe kali. Huu ni uhuni na ujinga mtupu.

“Sisi TDL hatuogopi ushindani, sio ushindani wa humu Tanzania, na nasema tutaendelea kuuza products zetu zinazozalishwa Tanzania, huko Uganda, Kenya south Sudan, Rwanda na Burundi, licha ya matatizo makubwa tunayopata, tutaendelea kuwasiliana na mabalozi, wa nchi husika, EAC office na wizara zenye mamlaka katika kukuza soko la pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki, kuhusu changamoto za kibiashara tunazozipata,” alisema Mgwassa.

Kama nilivyozungumza mwanzo sisi hatuzalishi Konyagi tuu, bali tunazalisha Zanzi cream, Knights, Viceroy brandy, siyo kwa sababu hatuwezi kuagiza, bali wka kutumia watanzania katika uzalishaji na kuwapa ajira. Msitufananishe sisi na watu wanaoleta makatoni ya pombe kutoka Ireland au uingereza, sisi tuko tofauti na mahitaji ya nchi hii tunayajua.

Rais wetu, Dk Jakaya Kikwete kila siku anasema issue hiyo hiyo, value added, value added, mbona masikio yenu mnafunga? Naomba niwaeleze ukienda South Africa leo utaona kila aina ya magari mapya, utaona Toyota, utaona Nissan utaona Mercedez benz, utaona Kia na kadhalika, lakini magari yote hayo yanaundwa South Afrika, huwezi kukuta gari imetengenezewa Singapore, nia ni kuhakikisha kuwa wenyeji wanapata kazi, na nia yetu TDL ni sawa na hawa.

Sioni kati ya nyie mtu ambaye anamchukua mtoto wake kumpeleka Nairobi au Dubai, kumtafutia kazi, wote mnawaleta kwetu, hata leo wengine wananiomba kazi, kwa hiyo naomba sana mtu akikujaza akili au upumbavu, na wewe jaribu kuchanganya na akili nzuri za kwako.