Kivumbi cha kutinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Kuendelea Leo

Dynamo-Kiev-Vs-Manchester-City-2

Nafasi nne za mwisho za michuano ya robo fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya – UEFA Champions League zitajulikana leo Jumanne na kesho Jumatano

Mmoja wa miamba wa soka la Ulaya atabanduliwa nje, wakati Bayern Munich itapambana na Juventus siku ya kesho Jumatano mjini Munich.

Bayern, mabingwa mara tano wa Ulaya wanastahili kuhakikisha kuwa viongozi wa ligi ya Italia Juventus hawatawaharibia kampeni yao baada ya timu hizo kutoka sare ya 2-2 katika mchuano wa mkondo wa kwanza.

Katika mechi nyingine ya Jumatano, Barcelona, wanaoongoza ligi ya Uhispania, wana faida ya mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Arsenal uwanjani Cam Nou. Barca haijashindwa mchuano hata mmoja katika mechi 37 mfululizo katika mashindano yote, na Arsenal inakabiliwa na kibarua kikali.

leo, Manchester City itashuka dimbani Etihad dhidi ya Dynamo Kiev ikiwa kifua mbele baada ya ushindi wake wa 3-1 katika mchezo wa kwanza. Atletico Madrid na PSV Eindhoven zitapambana katika mechi nyingine