Katika kuhakikisha ulimwengu wa soka unaendelea kutawala tanzania tayari mkoa wa arusha unatarajia kupata kituo kukubwa cha michezo sio kwa mkoani hapa pekee inawezekana tanzania nzima.
Kituo hicho kitakachoitwa TRUST St. Patrick Sports Academy kilichopo kitakuwa kinafundisha michezo kama vile, mpira wa miguu, riadha, mpira wa pete, mpira wa kikapu na tenis.
Mkurugenzi wa kituo hicho Patrick Khanya alisema kuwa tayari hosteli na viwanja kwa ajili ya kuwapika wachezaji hao zimekamilika hivyo kilichobaki ni kibali pekee ndicho wanachokisubili cha kuwaruhusu kuendesha michezo na kutambulika lasmi kiserikalini.
“Ukiacha viwanja vilivyotengenezwa tayari tumenunua eneo la hekali 10 ili kupanua zaidi na hii itasaidia kila mchezaji kujiweka bize katika fani yake, kwa mfano wale wanaocheza mpira wa pete, tenis kuna viwanja zaidi ya viwili kwa kila mchezo” alisema khanya.
Aliongeza kuwa kituo hicho kitakuwa kwa vijana walio na umri kuanzia miaka minne na kuendelea na kila kundi watakuwa kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya michezo katika kituo hicho Denis Shemtoe alisema kuwa kituo hicho kitakuwa kinakusanya vijana kutoka ndani na nje ya nchi ya tanzania ili kuongeza ufanisi wa kuinua michezo
Aliongeza kuwa mara baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwa ile ya kupata kibali cha serikali watakuwa wanaandaa mashindano mbalimbali ya michezo ikiwa ni njia moja wapo ya kuwapata wenye vipaji