Kipindi Kipya cha Nyumbani na Diaspora Ndani ya TBC1

Mjengwa Maggid

Mjengwa Maggid

NI kipindi kipya cha saa nzima chenye kuhusiana na Watanzania wa nyumbani na walio nje ya mipaka yetu. Ni kipindi daraja kitakachowaunganisha Watanzania katika kubaini fursa mbalimbali za kuinuka kimaendeleo, kwa mtu mmoja mmoja, jumuiya na hatimaye taifa.
Ni kipindi kitakachoongozwa na mchambuzi na mmoja wa wanahabari nguli nchini, Bw. Maggid Mjengwa. Jiunge naye kufuatilia mahojiano motomoto na watu wa kada mbalimbali kwenye masuala ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Ni kila siku ya Ijumaa saa 4 usiku na marudio Jumapili saa kumi jioni, hapa hapa TBC 1, ukweli na uhakika!