Sasa ‘Ongea na Janet’ inaonyeshwa katika Dstv kufuatia kuingia nao mkataba.
MO BLOG: Tulishuhudia uzinduzi wa ‘Ongea na Janet’ tukaanza kuona vipindi vikienda hewani hebu tuweke wazi yapi mafanikio uliyopata mpaka sasa..?
JANET: Mafanikio nilianza kuyaona kwenye vipindi 13 tu vya mwanzo ambavyo vilitengeneza ‘Season One’. Nashukuru Mungu ‘Ongea na Janet’ ilijulikana haraka sana, ikapata watazamaji wengi, ‘comments’ nazo zikawa nyingi, ‘changes’ zikawa nyingi nikajikuta kila ninapokwenda siitwi tena Janet naitwa ‘Ongea na Janet’.
Hilo lilikuwa ni fanikio la kwanza kwamba niliondoka kwenye media muda mrefu na niliporudi nikapokewa vizuri kwa hiyo nawashukuru kwanza watanzania wenzangu kwa hilo, nawashukuru sana mashabiki wa Janet kwa kunipa ‘love’ ukweli.
Lakini pia fanikio lingine lilikuja kujitokeza ambalo sikulitegemea kwa kipindi kile lilikuja kama ‘surprise’ kwangu kwani nikiwa sina hili wala line nikapata simu kutoka MNet-Dstv Nairobi wakaniambia kwamba shoo yangu wameipenda na wataichukua, wakati huo nikuwa nimesha ‘apply’ siku nyingi sana mpaka nimesahau.
Wakanipa na ‘amount’ nikakubali wakaniuliza unazo ngapi? Wakati huo ndio nimemaliza ‘Season One’ nikawaambia ziko 13 wakasema wangependa kama zingekuwa 26 nikasema sawa nitakaporudi ‘Season Two’ nitawapatia wakakubali.
Hivyo niliporudi ‘Season Two’ nikawa nimeingia kibiashara zaidi na Dstv wakawa wameni-‘support’ nikaweza kubadilisha set up nzima ya ‘Ongea na Janet’ na wakanipa hamasa zaidi na nikapata nafasi ya kuitangaza nchi yangu kwa na kwa sababu naoneka katika nchi nane (8) tofauti.
Pia nikagundua moja kwa moja kuwa sasa nimeingia kwenye ‘competition’ na watu nane wanaoziwakilisha nchi zao kwa maana ya kwamba Tanzania iko kwenye ‘competition’ ya ‘talk show’ na nchi nane za Afrika.
Mashabiki wangu nataka niwaambie kwamba nitajitahidi kuboresha kazi zangu na natamani Talk Show bora East and Central Africa itoke Tanzania.
Mmiliki na Mwendeshaji wa Kipindi cha Ongea na Janet Bi. Janet Sosthenes Mwenda katika moja ya vipindi walivyofanya na Bondia maarufu nchini Tanzania Japhet Kaseba.
MO BLOG: Ni nchi zipi ambazo ‘Ongea na Janet’ inaonekana Afrika..?
JANET: ‘Ongea na Janet ‘ inaonekana hapa nyumbani Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), hivyo naweza kusema ‘Ongea na Janet’ bado ina kazi kubwa ya kufanya si kwa ajili yangu bali kwa ajili ya watanzania wote.
MO BLOG: Baada ya kuingia mkataba na Dstv nini kilifuata..?
JANET: Baada ya kuingia mkataba nao fanikio la kwanza ilikuwa ni kubadilisha ‘set up’ ya kipindi kama nilivyosema na fanikio lingine ambalo lilikuwa ni ndoto yangu ya siku nyingi ni kuanzisha kampuni yangu mwenyewe ambayo itafanya vitu ambavyo natamani kuvifanya na tayari nimeshaifungua.
‘Soon’ itaanza ku-produce yenyewe kipindi cha ‘Ongea na Janet’, lakini sasa hivi tuko kwenye production ya kipindi kingine ambacho ni product ya ‘Ongea na Janet’ kwa hiyo watanzania wakae katika mkao wa kula kwani nitawaletea vipindi vingine viwili japo sita tangaza mimi.
Kwa sasa hivi kampuni yangu inafanya ‘production’ kwa hiyo nimekuwa na Media House, kwa mfano ukija na movie yako tunakurekodia, ukiwa na series zako tunakurekodia, dokumentari yako tunakutengenezea.
Kitu kingine namshukuru Mungu Dstv wamezidi kunifungulia milango kwani wamenifanya kuwa ‘agent’ wao kwa hapa nyumbani Tanzania. Kwa hiyo nimekuwa katikati ya mpishi na mlaji upande wa filamu, series na vipindi kwa hiyo kama kuna mtu sasa hivi ana kipindi anataka kiende Dstv anakileta kwangu, sisi tunakihariri upya, tunakifanyia ‘sub title’ kisha tunakipeleka Dstv.
Ilimradi hiyo kazi iwe ni ya kwake mwenyewe na ameisajili COSOTA.
Kusoma Mahojiano yote Bofya Hapa