Kipaji cha Mpira wa Miguu Chawabeba Ghana, Waingia Nusu Fainali

Kipaji cha Mpira wa Miguu Chawabeba Ghana, Waingia Nusu Fainali

KUPITIA televisheni za ITV na Clouds TV jana usiku katika kipindi cha 8 cha Guinness Football Challenge (robo fainali ya 3) Ghana waliweza kuibuka vinara na kupata dau kubwa zaidi tangu mashindano haya yaanze na kufuzu kuingia nusu fainali.

Jonathan Naab na Desmond Odaano kutoka Afika Magharibi waliweza kuhimili vishindo na vikwazo vyote hata kufikia hatua ya mwisho ya Ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia taslim dola za kimarekani 3,000 na kufanya kuwa na jumla ya dola 8,500 kutokana na dola 5,500 walizokua nazo awali.

Wawakilishi kutoka Ghana wataiwakilisha nchi yao katika nusu fainali pamoja na wawakilshi kutoka Kenya ambao nao wamefuzu kuingia nusu fainali Ephantus Nyambura na Samuel Papa, ambao pia walifanya vizuri ingawa hawakufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness.

Timu nne mpya zitaingia uwanjani katika robo fainali ya mwisho wiki ijayo nakuona kama wawakilishi wa mwisho kutoka Afrika Mashariki watatutoa kimasomaso na kufuzu kuingia nusu fainali

Robo fainali ya tatu ya Pan-African itarushwa kupitia televisheni za ITV na Clouds TV usikose kushuhudia timu kutoka Afrika Mashariki ikipambana vikali na nchi zingine za Afrika. Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki

Hakikisha unaufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.