Kiongozi wa Upinzania Auwawa Burundi

Raia wakiandamana nchini Burundi.

Raia wakiandamana nchini Burundi.


KIONGOZI wa chama kidogo cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi. Mwili wa kiongozi huyi, Zedi Feruzi pamoja na wa mlinzi wake ulipatikana nje ya nyumba yake kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura.

Mauaji ya mwanasiasa huyo yanafanyika wakati wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha kwa siku mbili maandamano yao dhidi ya Rais Pierre Nkurunziza kupinga uamuzi wake wa kuwania urais muhula wa tatu.

Uamuzi huo ambao wengine wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria umesababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua rais, maandamano ya wiki kadha na kukimbia kwa zaidi ya raia 100,000 kutoka nchini humo kwenda nchi za jirani.
-BBC