
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na kijana Ally Emmanuel ambaye Katibu Mkuu ameamua kumsomesha elimu ya ufundi katika Chuo cha Veta Shinyanga.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Maswa mkoani Simiyu na kuwaambia kwamba CCM inaahidi inachoweza kukitenda na wameshaanza kushughulika mambo muhimu kwa wilaya hiyo ukiwepo mradi wa umeme vijijini, maji, barabara na leseni za wachimbaji wadogo wa madini.