
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia na Khadija Kusaga aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, mara baada ya kuwasili Mjini Isaka Wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wa Chama wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana Akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama wakati alipowasili katika mji wa Isaka Wilayani Kahama leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kipaza sauti Katibu wa Itikadi , Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye wakati wakiongea na wananchi katika mji wa Isaka, katikati ni Khameja Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mapokezi hayo.
Khameja Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga akizungumza na wananchi wakati wa mapokezi hayo kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kulia ni Katibu wa Itikadi , Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye .