Kinana Azungumza na Waziri wa Masuala ya CPC wa China

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waziri anayeshughulikia masuala ya chama wa Chama cha Kikomnisti cha China, Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing, China. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa zwadi ya kinyagoo cha Kimakonde cha aina ya ‘Ujamaa’, Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo nchini China. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zwadi ya pambo la Kichina, na Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, Kinana alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo nchini China. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. (Picha na Bashir Nkoromo).