KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema Tanzania kuna wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi, lakini Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba wawekezaji walio wakubwa zaidi kwa tija ni wakulima.
Kinana alisema hayo Machi 20, 2013, wakati akizungumza na Mjumbe wa Tume ya Uongozi wa Taifa wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Liu Yunshan, mjini hapa, akiwa katika ziara ya kimafunzo nchini China, ambayo anafanya kwa mwaliko wa chama cha CPC, na amefuatana ujumbe wa watu 14 wakiwemo viongozi waandamizi na maofisa wa CCM.
Kinana alisema, kutokana na kutambua mchango mkubwa katika kuweza kuinua uchumi wa Tanzania, serikali ya Chama Cha Mapinduzi, imeanzisha na kuusimamaia mpango wa Kilimo Kwanza kwa lengo la kuwezesha wakulima walio wengi kuchangia uchumi wa taifa kupitia uwekezaji katika sekta hiyo na hiyo pia kuinua hali za vipato vyao.
Alisema, ili kupata mafanikio zaidi na ya haraka, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi itautumia uzoefu wa jinsi Chama Cha Kikomunisti cha kilivyoweza kuratibu na kusimamia kwa hali ya juu miradi ya kilimo hadi kuiwezesha China kuinuka kiuchumi njia kuu ikiwa ni kupitia sekta ya kilimomo.
Kinana alisema, alimwambia Liu, kwamba, Chama Cha Mapinduzi kinaona umuhimu wa kuiga uzoefu wa China katika kukuza uchumi kwa kuwa misingi ya kisiasa na na sera za Tanzania na nchi hiyo katika uchumi zinafanana kwa kuwa zinalenga zaidi kunua hali za wanyonge ambao ni wajasiramali wadogo wadogo katika uwekezaji kwenye shughuli mbalimbali na kilimo.
Alisema, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, kinakaribisha mataifa ya nje ikiwemo China kushiriki katika uwekezaji, lakini akabainisha kwamba uwekezaji ambao Tanzania inahitaji zaidi ni ule utakaonufaisha pande zote, Tanzania na nchi itakayohusika na kwamba baadhi ya faida ambazo inatarajia Tanzania kuzipata ni uwekezaji ambao utatengeneza nafasi nyingi za ajira kwa Watanzania.
Kuhusu siasa za nje, Kinana aalimwambia Liu kuwa, Chama Cha Mapinduzi kinasisitiza kama chama tawala, kwa kwamba Tanzania ni nchi huru hivyo haichaguliwi rafiki bali yenyewe ndiyo inayochagua kulingana na faida ambayo Watanzania wataipata, na haitafuata msukumo au mapendekezo ya taifa lolote la nje na kusisitiza kwamba Tanzania na China zina urafiki wa kihistoria tangu wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika.
“Na tutaendelea kuundumisha urafiki huu wa kindungu ulioanzishwa na waasisi wa mataifa yetu, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa upande wa Tanzania na hayati Mao Tsetung kwa upande wa China”, alisema Kinana na kuongeza;
“Tunaamini Tanzania inayo mengi ya kujifunza kutoka China kama ilivyo China nayo kuwa na mengi ya kujifunza kutoka Tanzania, tunaamini ziara ya Rais wa China Xi Jinping nchini Tanzania, itakayoanza (Jumamosi), mara baada tu ya kuchaguliwa rasmi kuwa rais wa nchi yake, ni alama muhimu ya namna chama cha kiongozi huyo ambacho yeye ni Katibu Mkuu, kinavyothamini uhusiano wake na CCM na Watanzania kwa jumla.
Alisema, kauli aliyotoa Rais Ping katiba Bunge Kuu la China, inayosisitiza nchi hiyo kuendelea kupambana na umasikiniu, kuondoa urasimu na umangimeza, kuimua hali za wananchi na kudumisha amani duniani inastahili kupongezwa na kila mpenda maendeleo duniani kote.
Kwa upande wake, Liu katika mazungumzo hayo, aliipongeza CCM kwa namna inavyoongoza, uongozi ambao amesema kutokana na umadhubuti umeweza kuifanya Tanzania kupiga hatua ya kubwa kiuchumi na kisiasa ambapo nchi imeendelea kuwa ya amani na utulivu na kuahidi CPC kuendeleza na kuimarisha uhusiano na CCM kwa manufaa ya serikali ya Tanzania na wananchi kwa jumla.
Alisema Tanzania chini uongozi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, imeweza kupiga hatua kubwa ingawa bado zipo changangamoto nyingi za kushughulikiwa na kueleza imani yake kwamba chini ya Rais Kikwete Tanzania itanedelea kuwa Umoja, amani na mshikamano vitasaidia kuleta maendeleo zaidi Tanzania.
Kiongozi huyo aliasa kuwa upo umuhimu wa kuimarushwa Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee kupambana na uninafsi, kujenga uaminifu na kutumikia wananchi kwa kufuata misingi mikuu ya uongozi bora. ” pia nakupongeza mheshimiwa Kinana kwa kuteuliwa kuwa katibu Mkuu wa Chama, naamini kuteuliwa kwako kumezingatia mchango mkubwa uliokwishatoa kwa taifa la Tanzania na uchapakazi wako.