Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kijiji cha Bunyambo wilayani Kibondo, Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Kaborou. (Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na msafara wake, wakinunua miwa njiani baada ya kukutana na muuzaji wa miwa hiyo, wakati wakitembea kwa mguu zaidi ya kilometa moja kwenda kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Bunyambo, baada ya kushiriki shughuli za ujenzi wa Ofisi ya CCM katika kijiji hicho, Wilayani Kibondo, Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma.(Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kumwambo, Wilayani Kibondo, Januari 31, 2013, baada ya kushiriki ujenzi wa chumba cha darasa, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma.(Picha na Bashir Nkoromo).
oFISI ZA tAWI