
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akisogeza matofali kwa Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi Siasa na
Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa kuyapandisha juu kwa ajili ya ujenzi wa soko la Mulugo
Market Mwambani lililopo katika ya kata Mwambani wakati viongozi hao
waliposhiriki ujenzi wa soko hilo linalojengwa na Mbunge wa jimbo la
Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Mh. Philip Mulugo
katika kuwakwamua kiuchumi wananchi wa jimbo la Songwe wilayani
Chunya, Kinana amemaliza ziara yake katika wilaya hiyo na kesho
anaanza ziara katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akishiriki ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika shule ya msingi ya
Saza katika kata ya Saza Mkwajuni Chunya, anayeshuhudia ni mkuu wa
mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro.
Wafugaji wa kijiji cha Mteka kata ya
Kapalala wilayani Chunya wakimpokea kwa ushujaa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
huku wakiimba nyimbo za kumsifu wakati alipowasili katika kijiji hicho
cha wafugaji.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Ndugu Deodatus
Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
kwa ajili ya kulnywesha mifugo yao lakini pia
kutumia kwa shughuli za kibinadamu kisima hicho kimefungwa mitambo
inayovutamaji kwa kutumia upepo Power Wind, kulia ni Nape Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Mbeya Mh. Godfrey Zambi.
wafugaji wakifurahia jambo wakati Kinana
alipokuwa akiongea nao.
Abdulrahman Kinana akiuliza jambo wakati
akikagua maradi huo katika eneo la matanki ya maji. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akimtwisha ndoo ya maji Gegwa Luhende mara baada ya kuzindua mradi
huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiongoza na wafugaji kuelekea eneo la kunweshea mifugo.
Mbunge wa jimbo la Songwe, Philip Mulugo
kushoto na mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro kulia
wakishiriki kazi ya kusomba tofali katika ujenzi wa bweni la shule ya
sekondari ya Kapalala wilayani Chunya,
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiwahutubiwa wananchi wa kijiji cha Udinde Mkwajuni.