Kinana Asema Watanzania Wataendea Kuiamini CCM ‘Milele’

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi baada ya kufungua tawi la CCM la Kitongoji cha Wangamiko, Kata ya Malangali wilaya ya Wanging’ombe, Machi 31, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji ilani ya Chama, na pia kukagua na kuimarisha uhai wa Chama katika mkoa wa Njombe.

Kinana akifungua ofisi ya CCM wilaya ya Makete

Na Bashir Nkoromo, Njombe

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, amesema ziara yake mkoani Njombe imempa imani kwamba CCM itaendelea kuaminiwa na wananchi kwa muda wa miaka mingi ijayo kuIongoza Tanzania.

Amesema imani hiyo ameipata baada ya kutembelea wilaya mbalimbali za mkoa huo na kushuhudia mwitikio mkubwa wa wananchi katika kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi, hadi katika maeneo ya vijijini ambayo ni magumu kufikika. Katika ziara hiyo ambayo anafuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Kinana ametembelea wilaya za Makete, Wanging’ombe, Ludewa, na Njombe.

Kinana alisema, changamoto iliyobakia kwa viongozi wa CCM ni kuwatembelea wananchi wa kawaida bila kujali kuwa ni wana CCM wenzao, ili kuzungumza na kusikiliza kero zao kwa lengo la kuzifanyia kazi, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi inakamilika kwa kiwango kilichotarajiwa.

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi baada ya kufungua tawi la CCM la Kitongoji cha Wangamiko, Kata ya Malangali wilaya ya Wanging’ombe, Machi 31, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji ilani ya Chama, na pia kukagua na kuimarisha uhai wa Chama katika mkoa wa Njombe. (Picha zote na Bashir Nkoromo).


Amesema, ili kuendeleza imani waliyonayo wananchi kwa CCM, ni lazima viongozi wa Chama na wale wa serikali, wajenge tabia ya kuwaeleza wananchi kinagaubaga kuhusu mafanikio au changamoto zinapojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo au huduma za kijamii.

Alisema, changamoto zinapojitokeza katika utekelezaji wa miradi au huduma za kijamii zozote, viongozi wa Chama lazima wawe na majibu ya kutosha kwa wananchi waliowatuma kazi na siyo na wao kugeuka walalamikaji kana wananchi ambao wanakuwa hawafahamu lolote kuhusu miradi.

“Linakuwa jambo la kushangaza kidogo, unakuta pahala fulani wananchi wanalalamika kuhusu kutokamilika mapema mradi fulani wa maendeleo, halafu unapomuuliza diwani wa eneo lile naye anashangaa badala ya kuwa na majibu ya kwa nini hali ipo hivyo”, alisema Kinana.

Alisema, wakati mwingine viongozi wanakuwa wanafahamu sababu ya changamoto zinazokuwa zimekabili miradi, lakini kutokana na hofu ya kupoteza kura za wananchi, wanaamua kukaa kimya na kujiunga na wananchi katika kulalamika.

Kinana aliitaka tabia hiyo kukoma kwa sababu lengi lililowafanya viongozi hao kuomba nafasi za kuongoza ni kuwa karibu na wananchi katika kuwaajulisha kila kinachoendelea na siyo vinginevyo.

Katibu Mkuu ambaye anatarajia kimaliza zoiara yake leo mkoani hapa, alirejea agizo lake la kuwataka viongozi wa CCM kuachana na tabia ya kupenda kuitwa waheshimiwa.

“Jamani viongozi tuwele mbele zaidi tumishi na siyo utukufu, mimi hadi leobado nmashangaa sana kwa nini viongopzi mnapenda sana kuitwa waheshimiwa. Nimeshalisema hili na hapa (Njombe) nakumbusha kwamba waca-CCM tuache kuitwa waheshimiwa tuitane Ndugu inatosha”, alisema Kinana na kuongeza;

“Sitaki kiugombana na wabunge, kama wao taratibu zinawalazimishwa kuitana waheshimiwa huko bungeni waacheni waendelee kuitana hivyo, lakini wana-CCM tusiitane hivyo”.