Kinana Aichana CHADEMA -Tunduma

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amebebwa juujuu na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akiwa amebebwa juujuu na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano
huo

1Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman
Kinana jioni ya leo, amefanya mkutano mkubwa wa hadhara mjini Tunduma,
ambao umehudhuriwa na maelfu ya wananchi. Katika mkutano huo
uliofabnyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, Kinana
aliambatana na majenbe ya Chama cha Mapinduzi , Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro, Katika mkutano huo Kinana amesema
wananchi kuikosoa CCM sio kosa kwani Chama hicho kimeingia mkataba na
wananchi pale kilipopewa ridhaa ya kuongoza nchi ili kutekeleza ilani
yake ya uchaguzi na ni haki ya mtu yeyote wakiwemo wapinzani ili kujua
maendeleo yao, Amesema CCM haitakubali kuona ukiritimba na umangimeza
wa baadhi ya watendaji Serikalini na unakwamisha maendeleo ya
wananchi, ameongeza kuwa kazi ya CCM ni kutenda tu na kazi ya
wapinzani ni kusema maneno tu.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-TUNDUMA-MOMBA
2Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akiwahutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini
Tunduma.
3Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia maelefu ya wananchi
waliojitokeza katika mkutano huo.
4Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akiwa amebebwa juujuu na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano
huo.
5Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisakata muziki na wakina mama wana
CCM kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
6Wananchi wakisakata muziki kabla ya
kuanza kwa mkutano.

7Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akiskata muziki na wananchi
9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana na ujumbe wake akilekea katika eneo la mkutano
10aMsafara ukiwasili mjini Tunduma
ukitokea wilayani Ileje
11 Maelefu ya wananchi wakishangilia
wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kianana hayupo pichani
alipokuwa akiwahutubia.
12Hapa akisisitiza jambo kwa wananchi
hao wakati akitoa hutuba yake
13Mzee wa kimila wa kabila la
wanamwanga wilayani Momba Jubeki Chipansia akimpa silaha za kijadi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kumsimika kuwa
miongoni mwa wazee wa kabila hilo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini Tunduma leo jioni.