
Meneja Miradi wa KIMD Constructor, Onesmo Nathan akimwelezea jambo kuhusiana na ujenzi wa daraja la watembea kwa Mguu la ITEBA linalounganisha Sinza na Manzese jijini Dar es Salaam linalojengwa na kampuni hiyo KIMD kutoka Mjini Kibaha mkoani Pwani. KIMD ni moja ya kampuni chache za Ujenzi zinazomilikiwa na wazawa kwa 100% na imekuwa ikifanya kazi nyingi za ujenzi wa barabara, mashule, na vituo vya afya katika maeneo mengi hasa Mkoani Pwani.