IDADI ya waliofariki dunia kutokana na Kimbunga kikubwa cha Sandy huko nchini Marekani imefikia 16 ambapo zaidi ya nusu ya vifo hivyo vimetokana na watu hao kuangukiwa na miti.
Vifo hivyo kwa ujumla wake vimeripotiwa katika majimbo ya New York, New Jersey, West Virginia, Connecticut, Pennsylvania na Maryland. Lakini kuna vifo vingine pia vimeripotiwa kutokana na kukatika kwa umeme na ajali ya gari katika balaa la kimbunga hicho.
Kuna ripoti ya mwanamke mwingine kufariki dunia kutokana na kimbunga hicho na mwili wake kuonekana ukielea katika maeneo ya bahari,huko Toronto nchini Canada jumapili. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha CNN Kimbunga hicho mpaka sasa kimeacha zaidi ya raia milioni 6.5 nchini Marekani pasipo nishati ya umeme katika eneo la Pwani ya Mashariki.
New York yaathirika zaidi
Vehicles are submerged on 14th Street near the Consolidated Edison power plant, Monday, Oct. 29, 2012, in New York. Sandy continued on its path Monday, as the storm forced the shutdown of mass transit, schools and financial markets, sending coastal residents fleeing, and threatening a dangerous mix of high winds and soaking rain. (AP Photo/ John Minchillo) Jiji la New York
New York ni miongoni mwa mji ulivurugwa vibaya na kimbunga hicho ambacho rekodi zinaonesha kiliambatana na mawimbi ya urefu wa meta 4 katika eneo la kusini la Manhattan. Katika eneo hilo maji yalifurika mpaka katika njia kubwa kabisa ya reli. Na soko la hisa la New York limeendelea kufungwa kwa siku ya pili mfululizo.
Duru nyingine zinaeleza kwamba moto uliowaka usiku kucha umeteketeza takribani nyumba 50 katika kitongoji cha Queens. Taarifa hizo zimesambazwa na kitengo cha zimamoto kupitia ukurasa wake wa Twiter ambapo hata hivyo hakikutoa maelezo zaidi kufuatia mkasa huo. Lakini kama inavyofahamika kwamba mkasa huo umetokea baada ya kimbunga Sandy kuyakumba maeneo ya Pwani ya Mashariki ya Marekani ukiwemo mji wa New York.
Hata hivyo balaa la kimbunga hicho bado halijafika kikomo ambako wasiwasi bado upo katika maeneo ya mbali ya majimbo ya Wisconsin na Ilinois. Ishara ya tahadhari imetolewa kuanzia Chicago mpaka Maine na Canada mpaka Florida. Tahadhari hiyo inaonesha kimbunga Sandy kitaendelea kuwa tatizo katika siku kadhaa zijazo na kitaambatana na mvua kali, theluji na mafuriko. Wakaazi walio katika eneo la Michigan na Ontario wametahadharishwa kuwepo kwa mawimbi makubwa. Na pia theluji zaidi kama ilivyo katika baadhi ya maeneo ya Atlantik ya kati.
Hali hiyo imezorotesha kampeni za uchaguzi wa rais wa Marekani ambapo Rais Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney wanafuatilia kazi ya uokozi katika maeneo ya yalikumbwa na kimbunga hicho.
-DW