Kilio cha huduma za maji Mkata Handeni

Muuzaji wa maji eneo la mkata akiwahudumia wateja wake huduma ya maji. Dumu moja la lita 20 ni sh. 500.


Baadhi ya wanafunzi eneo la Mkata wakiwa wamebeba ndoo za maji, haikujulikana kama maji hayo yalikuwa ni matumizi ya shule au vinginevyo.

UPATIKANAJI huduma ya maji kwa wakazi wa Kata ya Mkata Wilayani Handeni bado ni tatizo. Hali hiyo imewafanya wakazi wa eneo hilo kununua maji sh. 500 kwa dumu maji ambayo pia usalama wake ni mdogo kulingana na yanakopatikana. Wakizungumza na mtandao huu juzi baadhi ya wakazi wa eneo la Mkata walisema hutegemea maji ambayo hupatikana Mto Mbwewe uliopo kilometa 30 kutoka eneo hilo, maji ambayo huuziwa kwa sh. 500 kwa dumu moja la lita 20.
Chanzo: www.thehabari.com