Kilimanjaro Stars Yarejea Dar, Kim Poulsen Kutaja Kikosi cha Taifa Stars

Kilimanjaro Stars ikiwasili jijini Dar es Salaam kutokea Uganda. (Picha na Shafii Dauda Blog)

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen kesho Desemba 10, 2012 saa 6 kamili mchana ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) atatangaza kikosi chake kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12, 2012 jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22, 2012 katika Uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura iliyotolewa kwa vyombo vya habari alisema baada ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kumaliza kushiriki mashindano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, imerejea Dar es Salaam Jumapili ya Desemba 9, 2012 hivyo Poulsen anatarajiwa kutaja kikosi kimpta cha Taifa Stars.