Kikwete Hana Mamlaka Kuvunja Bunge la Katiba – Jaji Werema

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi wa masuala Kisheria  kwa waandishi wa habari kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo

Na Rose Masaka – MAELEZO

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema Rais wa Tanzania hana mamlaka ya kulivunja Bunge la Katiba kisheria. Kauli hiyo imetolewa ikiwa ni siku chache baada ya wabunge wa kundi la UKAWA kumtaka Rais Kikwete kulivunja bunge hilo baada ya wao kugoma kuendelea na vikao vya bunge hilo.

Aidha Mwanasheria huyo wa Serikali amewataka viongozi wa vyama vya siasa waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba (UKAWA) kurejea bungeni ili kufanya maridhiano ndani ya bunge hilo.

Jaji Werema alisisitiza kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza rais kulivunja bunge hilo kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza bunge.

“Sheria inasema bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba kupatikana, kinyume na hapo bunge husitishwa kufikia maridhiano na kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia,” alisema Jaji Werema.

Pia Jaji Werema alisema kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kuweza kupata katiba iliyo bora kwa nchi na watu wake.

Aidha, Jaji Werema aliviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji wa taarifa na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza kusaidia nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.