Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia jiwe la msingi mara baada ya kuzindua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza katika hafla hiyo jana
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44..
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoka ndani ya nyumba ya mfano baada ya kuzindua nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meneja wa NHC mkoa wa Dodoma Itandula Gambalagi wakati wa uzinduzi wa nyumba hizo za gharama nafuu.
Na Sifa Lubasi, Kongwa
HALMASHAURI nchini zimetakiwa kununua nyumba za bei nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) ili kuwapangisha watumishi wake. Kauli hiyo ilitolewa jana na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizindua mradi wa nyumba nafuu katika eneo la Mnyakongo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya maeneo watumishi wa halmashauri kukaa mbali na sehemu zao za kazi kwa visingizio vya kukosa makazi. Alisema sababu hiyo sasa haina msingi katika maeneo ambayo NHC imejenga nyumba zao kwani halmashauri inaweza kununua nyumba hizo na kuwapangisha watumishi wake.
‘’ Hawa NHC wana utaratibu kwa kupitia mabenki wanayoshirikana nayo hivyo kwa kutumia utaratibu huo halmashuri mnaweza kwenda katika hizo benki na kuingia mkataba na kukopa nyumba hizo na kisa kuwapangisha watumishi…’’ alisema.
Aidha Rais Kikwete alisema shirika hilo linafanya kazi nzuri katika ujenzi wa nyumba hizo za bei nafuu huku akilitaka kuongeza zaidi idadi ya nyumba. Alisema ni vyema sasa halmashuri zikaongeza maeneo ya kujenga nyumba hizo ili wananchi wengi zaidi waweze kuishi katika nyumba bora.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NHC Nehemia Mchechu alisema mradi huo ni utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Alisema mradi huo wenye nyumba 44 hadi kukamilika utakuwa umegharimu Shilingi bilioni 1.2.
Alisema nyumba hizo zinauzwa kwa gharama kati ya Sh milioni 35 hadi 40 kulingana na ukubwa wa nyumba husika.
Hata hivyo alisema bado kuna tatizo la kodi katika uuzaji wa nyumba hizo na ndio kinachofanya kuuzwa kwa bei kubwa.
Alimuomba Rais kusaidia katika kusukuma nia ya kushusha kodi ili nyumba hizo ziuzwe kwa bei nafuu na kila mwananchi aweze kununua.
(Picha zote kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)