Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewateua mabalozi wawili kuiwakilisha Tanzania nchini Italia pamoja na Naibu Balozi wa kudumu Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York.
Taarifa hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam, licha ya uteuzi kufanyika tangu Oktoba 12, mwaka jana, 2011. Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Yohana amesema; kuwa Rais Kikwete amemteua Dk. James Alex Msekela kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia. Kabla ya hapo Msekela alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Aidha, taarifa hiyo ya Sefue imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Naibu Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York. Kabla ya hapo, Mwinyi alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Katibu Mkuu kiongozi amesema katika taarifa yake kuwa wateuliwa hao wawili wataapishwa Januari 5, 2012.