Kikosi Cha Wachezaji Bora wa Euro 2016

Wachezaji wa Portugal wakishangilia na kombe lao

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, anayechezea Real Madrid ya Uhispania, ni miongoni mwa wachezaji walioorodheshwa kwenye kikosi bora cha michuano ya Euro 2016 kilichotangazwa na Shirikisho la Soka Ulaya, Uefa.
Ronaldo aliwahi kujumuishwa katika kikosi sawa mwaka 2004 na mwaka 2012.

Raia mwenzake, Pepe pia yupo kwenye kikosi hicho na aliwahi pia kujumuishwa 2008 na 2012.
Awali, kulikuwa kukitajwa kikosi cha wachezaji 23 lakini wakati huu kumetajwa kikosi cha wachezaji 11.

Eder: Mchezaji aliyeliza Wafaransa

Kikosi kamili kinajumuisha (4-2-3-1): Rui Patrício (Ureno); Joshua Kimmich (Ujerumani), Jérôme Boateng (Ujerumani), Pepe (Ureno), Raphaël Guerreiro (Ureno); Toni Kroos (Ujerumani), Joe Allen (Wales); Antoine Griezmann (Ufaransa), Aaron Ramsey (Wales), Dimitri Payet (Ufaransa); Cristiano Ronaldo (Ureno).
Kikosi hicho kiliteuliwa na jopo la kiufundi cha Uefa lililojumuisha, miongoni mwa wengine, Sir Alex Ferguson na David Moyes.

“Tunaamini kikosi hiki cha wachezaji XI kinawakilisha wachezaji bora zaidi walioshiriki michuano,” amesema, Ferguson, ambaye ni balozi mwema wa ukufunzi wa Uefa.