Serikali ya Burkina Faso imevunja kikosa cha kumlinda rais ambacho kiliwashika mateka mawaziri wakati wa majaribio ya mapinduzi yaliyofeli.
Hatua hiyo ilichukuliwa wakati wa mkutano wa kwanza wa serikali tangu siku ya Jumatano wakati rais wa mpito Michel Kafando aliporejeea madarakani.
Image copyrightAFP
Image caption
Burkina Faso
Waziri wa masuala ya ulinzi amefutwa kazi na tume imebuniwa kuwatambua wale waliohusika katika kupanga mapinduzi hayo.
Takriban watu 19 waliuawa wakati wa maandamano ya kupinga mapinduzi hayo.
-BBC