Timu za Ligi Kuu ya Uingereza zimefanikiwa kutoa wachezaji wawili, sawa na ligi ya Ujerumani na ile ya Ufaransa katika Kikosi bora cha wachezaji kumi na mmoja kilichocheza hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kikosi hicho kimetangazwa na UEFA huku jambo la kushangaza wengi ni kuachwa nje kwa nyota wa Barcelona Lionnel Messi, Neymar na Luis Suarez.
Katika kikosi hicho Washambuliaji ni Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Hulk (Zenit St Petersburg) pamoja na Thomas Muller (Bayern Munich) ndio wanaoongoza safu ya ushambuliaji, kikosi hicho kikitumia mfumo wa 4-3-3.
Kutokana na kikosi hicho inamaana Mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Barcelona, hawajatoa hata mchezaji moja katika kikosi hicho licha ya kuwa na safu kiwembe ya ushambuliaji.
Kikosi kamili ni:
Kipa: Kevin Trapp (PSG)
Mabeki: Andrea Barzagli (Juventus),Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Diego Godin (Atletico Madrid), David Alaba (Bayern Munich)
Viungo wa Kati: Sven Kums (Gent), Willian (Chelsea), Raheem Sterling (Manchester City)
Washambuliaji: Thomas Muller (Bayern Munich), Hulk (Zenit St Petersburg), Cristiano Ronaldo (Real Madrid).