Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kumpongeza Mwakilishi mpya wa Jimbo la Bububu Hussein Ibrahim Makungu, (kulia) CCM, kwa kushinda uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar, kushiriki katika kikao cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, kilichofanyika. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]
Makamo Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk. Ali Mohamed
Shein, (wa pili kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Balozi Seif Ali Iddi, (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, kwa pamoja wakiwa wamesimama
kabla ya kuanza kikao cha siku moja cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]
Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa katika kikao cha siku moja chini ya Mwenyekiti wake, Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, wakiwa katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar, kilipofanyika kikao hicho. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]