Kijiji cha Ngareni Rombo Chaomba Umeme

Usambazaji umeme

Usambazaji umeme

WAKAZI wa Kijiji cha Ngareni Kata ya Ngoyoni Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wameliomba Shirika la Kusambaza Umeme (TANESCO) kupelekewa huduma ya umeme jambo ambalo linawasababishia kuzorota kwa maendeleo katika kijiji hicho.

Diwani wa Kata hiyo Protas Lyakurwa Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wakati alipokua akichangia taarifa ya Shirika la kusambaza umeme iliyowasilishwa na Meneja wa TANESCO, Wilaya ya Rombo, Rajabu Haule alimwomba kusogeza huduma hiyo katika Kijiji cha Ngareni kwani ni kijiji pekee Wilaya ya Rombo ambacho hakijafikiwa na umeme.

Alisema kuwa zaidi ya wananchi 196 walishajaza fomu ya kuomba kufungiwa umeme na kulipia lakini hadi sasa bado hawajafungiwa. Aidha mmoja wa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Rombo, alilamikia vitendo vinavyofanywa na Tanesco wilayani Rombo kwa kukata umeme bila kutoa taarifa kwa wateja wake jambo ambalo linasbabisha usumbufu mkubwa kwa wateja.

Alilitaka shirika hilo kuwa na utaratibu maalumu wa kutoa taarifa ya kukata umeme kwani inawapa wateja wake utayari badala ya kukata bila kutoa taarifa ambapo wakati mwingine hali hiyo inasababisha hasara. Awali meneja wa Shirika la kusambaza umeme (TANESCO) wilayani Rombo, Rajabu haule akiwasilisha taarifa ya shirika hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma hiyo pamoja na kuwaunagnisha wateja wapya japo si kwa kiwango cha kurizisha kutokana na kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wanguzo na nyaya.

Haule aliwataka wateja wapya walioomba kuunganishiwa huduma hiyo wawe wavumilivu kwani jitihada zinaendelea