Na Rungwe Jr.
California, CA
Juma hili Kamera ya dev.kisakuzi.com ilikuwa maeneo ya Lompoc, California, na kubahatika kukutana na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Derek, akiwa na Farasi wake. Kama ilivyo ada, dev.kisakuzi.com ili amua kumuuliza maswali mawili matatu kufahamu kulikoni Farasi yupo kwenye maeneo mbayo ni maegesho ya Magari!? Kijana Derek alinifahamisha kuwa yupo maeneo hayo kumtembelea rafiki yake na aliamua atumie Farasi kama usafiri kutokana na kwamba ana miliki BMW (X5), ambalo hivi karibuni imemuwia vigumu kulitumia kutokana na bei kali za mafuta hapa California na Marekani kwa ujumla.
Mpaka sasa California ndio mji unaolipa bei za juu za mafuta kuliko miji mingine yote Marekani. Kwa mujibu wa gazeti la “The Washington Post” wateja wa California, Washington, Illinois na miji mingine mitano hapa Marekani, wanalipa bei za juu za mafuta kwa wastani wa dola 3.91 – 4.21 kwa lita. Pamoja na wastani huu, Siku ya Jumatano (yaani Jana) dev.kisakuzi.com, ilishuhudia bei za mafuta katika miji ya Ventura, Santa barbara, na Lompoc ikiwa ni kati ya dola 4.25 – 4.79. Kwa bei hizi, uendeshaji wa magari umekuwa ni bughudha kubwa mifukoni.Hata hivyo, bei za mafuta zinatarajiwa kushuka sana katika siku chache zijazo, haswa kuanzia kipindi hiki cha sikukuu ya “Kumbukumbu” (Memorial Day), ambayo mwaka huu imeangukia katika siku yake maalum, yaani Mei 30 (May 30th ). Hivyo basi, Wamarekani wana mapumziko marefu ya mwisho wa wiki kuanzia Ijumaa hadi Jumatatu, na hatimaye kurudi mzigoni siku ya Jumanne.